UHONDO WOTE

DIVA: ZITTO NI MUME WANGU


MTANGAZAJI wa Kipindi cha Ala za Roho ‘Diva’ kwa mara ya kwanza, amejilipua kuzungumzia uhusiano wake na Zitto Kabwe kwamba walikuwa mke na mume. Katika mahojiano maalum na mwanahabari wetu jijini Dar juzi, Diva alisema anashangazwa na baadhi ya vyombo vya habari (siyo vya Global Publishers) kumnyima uhuru wa kuongelea suala lake na ‘zilipendwa’ wake huyo wakati kisheria yeye ni mke wake hivyo anapaswa kuzungumzia kutengana kwao. MSIKIE DIVA “Ninyi mnayaongelea mambo ya Zitto na mimi juu kwa juu tu hamjui kama mimi nimeishi naye kama mke na mume nyumbani kwake Masaki (Dar), sasa nini kilisababisha penzi letu kuvunjika watu hawajui, nina ushahidi wa kutosha lakini wanaongeaongea tu,” alisema Diva.Akaongeza: “Sasa ninavyojua mimi kwa sheria za nchi, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita tayari ni mke na mume. Hawezi kuniacha kirahisirahisi tu.” KIPINDI CHAZUA BALAA Diva alikwenda mbele zaidi kufuatia kauli ya Zitto aliyoitoa hivi karibuni kupitia Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani na Runinga ya East African Television ‘EATV’ na mtangazaji Salama Jabir. Zitto aliulizwa ana uhusiano gani na Diva, naye akajibu ni mtu wanayefahamiana tu lakini si mpenzi wake. HASIRA ZA DIVA Ilidaiwa kwamba, majibu hayo ya Zitto kwa Salama ndiyo yaliyoibua hasira ya Diva hadi kufikia hatua ya kutupia kwenye ukurasa wake wa Instagram, e-mail aliyodai aliwahi kutumiwa na Zitto siku za nyuma akimtaka asiwe anaweka wazi uhusiano wao kwa sababu atachafuka kisiasa.mkaimalizie nimeiweka www.jipange101.com Bonyeza link kwa my bio hapo juuu owk bayiiii👣👣👣
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Share Story hii:

Facebook Google+ Twitter

0 Response to "DIVA: ZITTO NI MUME WANGU"

Post a Comment