![]() |
Basi la Upendo Coach likiwa limegonga kwa mbele |
Ajali mbaya imetokea asubuhi hii ikihusisha mabasi mawili ya kampuni ya Super Feo likitokea Dodoma kuelekea Songea na basi la Upendo Coach kutokea Dodoma kuelekea jijini Mbeya.
Taarifa nilizopata kutokea eneo la tukio zinasema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni punda aliyekuwa akikatisha barabara na mwendo kasi wa basi la Upendo bila umakini wa dereva wa basi hilo.
Abiria wa basi la Upendo wamelalamika kuwa mwendo kasi wa gari lao ambapo dereva alikuwa akilifukuzia (ligi) basi la Super Feo kwa kasi ya ajabu bila kuacha nafasi ya usalama baina ya basi moja na jingine.
Hali hiyo ilipelekea ajali kutokea pale dereva wa basi la Super Feo aliposimama ghafla kuepuka kugonga punda aliyekuwa akikatisha barabarani.
Inasemekana dereva wa basi la Upendo amevunjika miguu na abiria wengine wamejeruhiwa vibaya.
Basi la kampuni ya Super Feo likiwa limebamizwa nyuma
0 Response to "MZIMU WA AJALI: BASI LA UPENDO COACH NA SUPER FEO YAGONGANA LEO"
Post a Comment