UHONDO WOTE

MTUME PETER RASHID ABUBAKAR AOA MKE WA PILI


Mtume Peter Rashid Abubakari, kiongozi wa kanisa la RGC lililoko Mbezi Kimara Dar Es Salaam, ameamua kumuacha mke wake Bi Zuwena (Catherine) aliyeoana naye tangu mwaka 1985.

 Alipohojiwa inakuwaje kwa nini amuache na kumuoa Pamela Didas Asenga, binti mdogo wa miaka 20, alidai ndoa yake hiyo ya mwanzo haikuwa halali kwa kuwa alioa akiwa bado mwislamu na alifungishwa na shehe! Kwa hiyo mungu amemfunulia na amempa mke mwingine mwema! 

 Ndoa hiyo ilifungwa tarehe 29/08/2014, ilifungishwa na Askofu Innocent Lugagi, wa kanisa la White House la Durban Afrika Kusini! Mtume Peter Rashid Abubakar baada tu ya kutoka kufunga ndoa yake South Afrika amerudi nchini Tanzania na Jumapili akiwa kanisani kwake awatangazia waumini wake kuwa kama una mke ambaye mlichukuana wakati wa ujinga wenu na umekaa naye miaka mitatu au zaidi na hana tabia ya kimungu mkorofi na mchokozi na hujafunga naye ndoa ACHANA NAYE ILI MUNGU AKUPE MKE MWEMA. 

Na mwanamke naye vilevile. Alipohojiwa na mmojawapo wa marafiki zake aliyeshangazwa na tukio hilo, kwenye ukurasa wake wa Facebook mtume huyo alijibu hivi: “…… tafsiri ya mke ni yule uliyefunga naye ndoa kanisani au kwa DC 1Kor 7:15. Huyo nilikuwa nazini naye tu!! Mungu aliponifunulia siri hiyo nikatubu na kumuomba Mungu anipe mke mwema na amenipa.”

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Share Story hii:

Facebook Google+ Twitter

0 Response to "MTUME PETER RASHID ABUBAKAR AOA MKE WA PILI"

Post a Comment