UHONDO WOTE

MGANGA AMUUA MWANAYE KISA KAZALIWA KATANGULIZA MAKALIO

MTOTO Regina Geofrey (miezi 14), ameuawa kwa kunyongwa na baba yake mzazi Geofrey Kilingwa ‘Simbaiwe’ (27), kwa madai alizaliwa akiwa ametanguliza makalio yake.
Baba wa binti huyo ambaye pia ni mganga wa kienyeji anayeishi kitongoji cha Mwikang’ombe, Kijiji cha Katuma, Mpanda, alitenda unyama huo kwa madai mtoto aliyezaliwa kwa kutanguliza  makalio ni mkosi na nuksi kubwa katika shughuli zake hizo za uganga wa kienyeji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa,  mzazi huyo  aliyetenda uhalifu huo Julai 20 mwaka huu ambako alikamatwa na Jeshi la Polisi Agosti 26 mwaka huu.
Inadaiwa kuwa, siku hiyo ya tukio, mtuhumiwa baada ya kumnyonga hadi kufa binti yake huyo, alimzika kwa siri katika  kibanda chake anachofanyia shughuli zake za uganga wa kienyeji.
TANZANIA DAIMA
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Share Story hii:

Facebook Google+ Twitter

0 Response to "MGANGA AMUUA MWANAYE KISA KAZALIWA KATANGULIZA MAKALIO"

Post a Comment