UHONDO WOTE

FIESTA YA HAIRISHWA KUTOKANA NA AJALI MBAYA ILIOHUSISHA MABASI MAWILI MKOANI MUSOMA NAKUSABABISHA VIFO VYA ZAIDI YA WATU 60

Kwamujibu wa Mtangazaji wa Clouds GEA HABIBU;

"Kufwatia ajali mbaya inahusisha mabasi mawili mkoani musoma nakusababisha vifo vya zaidi ya watu 60...Leo Serengeti fiesta haitofanyika tena mkoani musoma mpaka itakapo tangazwa tena.Mwenyezi mungu awapumzishe kwa amani wote waliopoteza maisha katika ajali hiyo" VIA Instagram
UPDATE!!!
AJALI YAUA 39 BUTIAMA: Takribani watu 39 wamefaraki na majeruhi zaidi ya 79 asubuhi leo baada ya mabasi ya Mwanza Coach na J4 kugongana eneo la Sabasaba huko Butiama, Mara. 

Ajali hiyo ilihusisha basi la Mwanza coach lenye namba za usajili T 736 AWJ na basi la JK express lenye namba za usajili T677 CYC. Taarifa za awali zinasema chanzo cha ajali kilitokana gari ndogo aina ya Nissan yenye namba za usajili T 332 AKK. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali wilaya ya Musoma mkoani humo na majeruhi wanaendelea kutibiwa hospitali hapo.




NEXT PHOTOS

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Share Story hii:

Facebook Google+ Twitter

0 Response to "FIESTA YA HAIRISHWA KUTOKANA NA AJALI MBAYA ILIOHUSISHA MABASI MAWILI MKOANI MUSOMA NAKUSABABISHA VIFO VYA ZAIDI YA WATU 60"

Post a Comment