MSANII nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz,’ mwishoni mwa wiki alinusurika kichapo kutoka kwa mashabiki wenye hasira wakikerwa kuchelewa kwake kupanda jukwaani kutumbuiza, mjini Stuttgart, Ujerumani.
Diamond alikumbana na kisanga hicho baada ya kushindwa kupanda jukwaani kwa wakati mbele ya mashabiki waliokuwa wamelipa kiingingilio cha euro 25 kusjionea shoo iliyokuwa ianze saa 4:00 usiku.
Habari kutoka nchini humo zinasema, licha ya shoo kutakiwa kuanza muda huo, Diamond alishindwa kufanya hivyo badala yake akatinga ukumbini saa 10 alfajiri.
Akiwa na promota wake aliyejulikana kwa jina la Britts Event, raia wa Nigeria, alipokelewa na chupa za mashabiki wenye hasira waliokuwa wamekerwa kumsubiri msanii huyo kwa saa sita zaidi.
Baadhi ya mashabiki wakiwa na hasira kali, waliona kurusha chupa hakutoshi, hivyo kuamua kuvamia jukwaa wakitaka mkumchapa Diamond na promota wake.
Habari zinasema, kilichowakera washabiki sio msanii huyo kuchelewa tu ukumbini, pia ubovu wa vyombo vya muziki ambapo kwa hasira, waliamua kuvunja vyombo na kuwashambulia madj.
Katika vurumai hiyo, madj walijeruhiwa hadi kukimbizwa hospitalini kwa matibabu ambako wamelazwa hadi sasa huku mmoja wa madj akipoteza kompyuta mpakato (lapotop)
Katikati ya kisanga hicho, Dj Flor alipatwa na mshtuko wa moyo hadi kukimbizwa hosptalini huku mwingine Dj Drazee akipata kipondo na amelazwa akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini.
Kwa mujibu wa Polisi wa nchini ujerumani, ni mara ya kwanza kutokea kwa tukio la aibu hiyo kwa msanii kukawia kufika jukwaani hadi mashabiki kushikwa na hasira.
Alisema hiyo ni kutokana na utamaduni wa raia wa Ujerumani kuheshimu muda, hivyo kitendo cha Diamond kuwaweka ukumbini kwa zaidi ya saa sita, kiliwakera mno.
Habari zinasema, hadi sasa polisi nchini Ujeruamni, wanamtafuta mwandaaji wa shoo hiyo na kufanya tathmini kujua thamani ya uharibifu uliofanywa na mashabiki.
Baada ya kukamirisha yote hayo, polisi itamfikisha promota huyo mahakamani kwani anakabiliwa na tuhuma za kujihusisha na mtandao wa kibiashara.
Akielezea kisa hicho kupitia mitandao ya kijamii, Diamond alikiri kutokea kwa kisanga hicho huku akimtupia lawama promota wake kwani ndie aliyekuwa akimweleza muda bado wa kupanda jukwaani.
Kwa upande wa meneja wake wa hapa nchini, Babu Tale amessema tukio hilo limesababishwa na promota wa shoo hiyo ambaye alilenga zaidi kuangalia wingi wateja ukumbini kwa lengo la kuuza vinywaji.
TANZANIA DAIMA
0 Response to "DIAMOND ANUSURIKA KICHAPO UJERUMANI"
Post a Comment