UHONDO WOTE
Showing posts with label SIMULIZI. Show all posts
Showing posts with label SIMULIZI. Show all posts

SIMULIZI: NAMNA FREEMASON ILIVYOINGIA TANZANIA

Mwandishi wa simulizi hizi, Sir Andy Chande, ambaye ni kiongozi mstaafu wa Freemason Afrika Mashariki, jana alieleza namna chama hicho kilivyoingia nchini mwaka 1903 na kufungua ofisi ya kwanza huko Zanzibar. Sasa endelea...

Wakati ule, hata hivyo, Ofisi ya Freemason Afrika Mashariki ilikuwa imetoa mchango mkubwa katika kusaidia kuimarisha ufreemason katika sehemu za bara.
Hatua ya kwanza ya Freemason ilikuwa ni kuimarisha uchumi, biashara na shughuli za kisiasa. Baadaye nguvu ikaelekezwa zaidi eneo la bara la Afrika Mashariki, siyo kwa Wajerumani wa Afrika Mashariki, bali kwa Wakenya, ambapo kukamilika kwa ujenzi wa reli ya Uganda kulikuwa tayari kumeanza kuonyesha matokeo mazuri katika eneo kubwa lililokuwa makazi ya wazungu Afrika Mashariki.
Zanzibar ilikuwa tayari imeshapiga hatua nzuri katika masuala la kilimo, biashara na miundombinu wakati huo.
Mwaka 1901, bidhaa ya kwanza ya majani ya chai Afrika Mashariki ilitengenezwa huko Dunga.  Mwanzoni majani hayo yalilimwa kwenye bustani iliyoanzishwa mwaka 1899.  Majani yalikuwa yakitengenezwa kwa kutumua zana za mikono, kuanikwa juani na kukaangwa kwa kutumia jiko la kawaida la mkaa.
Baadaye mwaka uleule, kiwanda cha kwanza cha mafuta kilianzishwa Zanzibar kikifuatiwa na ujenzi wa tangi katika mji wa Mtakuja. Tangi hilo lililowekwa na Messrs Smith Mackenzie na kampuni yake kama wakala wa Kampuni ya usafirishaji na biashara ya Shell Ltd, lilikuwa kwa ajili ya kukusanya mafuta mengi.
Pia kampuni hiyo ilijenga kiwanda kwa ajili ya kutengeneza mapipa ya kuwekea mafuta ya taa.
Mwaka 1903, gazeti la kwanza huko Zanzibar lililojulikana kama “Samachar” lilichapishwa. Baadaye gazeti hilo lilikuwa likichapishwa kila siku, huku chapisho lake la kwanza likitoka Agosti 21, 1905. Baadaye magazeti mengi tu yalichapishwa Zanzibar.
Mwaka 1903, nyumba nzuri zilijengwa Kigomasha huko Pemba na Chumbe. Mwaka uliofuata, Freemason Kenya waliomba kupewa hati ya kutambuliwa ili waanzishe ofisi.
Ofisi hiyo Namba 3084 ilifunguliwa rasmi Mei mosi, 1905. Baadaye, ilipandishwa ngazi ya juu zaidi. Mimi ni mwanachama katika ngazi hiyo.
Sultani wa Zanzibar alisisitiza ujenzi wa miundombinu. Ufaransa walifungua ofisi ya posta iliyokuwa ikitoa stempu za aina mbalimbali baada ya kuwepo zilizotolewa na nchi hiyo kati ya mwaka 1870 na 1900.
Shule ya familia ya kifalme na Waarabu daraja la pili ilifunguliwa, huku kampuni ya Marekani ikijenga njia ya reli kuunganisha Bububu na Forodhani na baadaye kuiuzia Serikali mwaka 1911.
Mwaka 1905, nyaya za umeme zilifungwa umbali wa maili tano kuzunguka kasri la mfalme. Kazi hiyo ilifanywa na Mr J.A. Jones wa New York.
Kitu cha kuvutia, mitaa ya Zanzibar ilikuwa na umeme mapema zaidi kuliko mitaa ya London, ambako walikuwa bado wanatumia taa za gesi.
Kampuni ya Marekani ilifunga huduma ya simu katika kituo cha simu cha Old Fort na Ofisi ya Posta huko Shangani.
Hata hivyo, huduma za posta ambazo zilikuwa zimeanza mwaka 1873 katika jengo la Mackenzie zilikuwa tayari zimeunganishwa na umoja wa posta.
Reli  ya Uganda ilikuwa imeanzisha njia ya kuimarisha ukoloni zaidi katika eneo la bara. Jambo hili lilileta maendeleo na kuanzishwa kwa makazi mapya Kenya na Uganda.
Kadri ya muda ulivyokwenda, baadaye maeneo hayo yalikuja kuwa vituo muhimu vya Freemason kukua na kupanuka katika eneo lote la Afrika Mashariki.
Ofisi ya Freemason namba 3084 ilifanya kazi nzuri sana. Kazi ya kwanza ya Freemason mjini Nairobi ilikuwa kuhakikisha idadi ya wanachama inaongezeka.
Katika kufanikisha jambo hilo, ofisi iliamua kuwapandisha ngazi wanachama wote katika mkutano mmoja jambo ambalo linazuiwa na katiba ya Freemason.
Ofisi iliweka makazi yake ndani ya jengo la Posta katika mtaa wa Victoria (siku hizi unaitwa Tom Mboya). Ilikuwa ikitumia kinanda ilichoazima kutoka Kanisa la Mtakatifu Stefano. Ofisi hiyo ikiwa chini ya mwangalizi kutoka Scotland, ambaye ofisi yake iliitwa Scotia namba 1008, ilianzishwa mwaka 1906.
Kijana mdogo mwanachama katika ofisi ya Harmony aliteuliwa kuwa mkuu wa kwanza wa ofisi ya Scotia. Kutokana na ofisi ya Harmony kuisaidia ofisi ya kwanza ya Scotland wakati wa kufanya sherehe zao, utamaduni na mambo mengine, utaratibu huo ulizoeleka kwenye mfumo mzima kiasi cha kuleta utata kwa wanachama wa Freemason kati ya ofisi hizo mbili.
Kwa miaka mingine sita, Sir Charles Bowring, ambaye alitumika kama gavana wa makazi awamu  tatu, alitoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya Freemason Kenya na Uganda.  Alikuja kuteuliwa kuwa Mkuu wa kwanza wa uchaguzi kwa nchi za Afrika Mashariki.
Miaka miwili baadaye, mwaka 1909 na 1910, yalitokea mambo makubwa mawili ambayo yalionyesha ukuaji wa Freemason Afrika Mashariki. Septemba 1909, ofisi ya Harmon namba 3084 ilipewa heshima ya kutembelewa na Rais wa Marekani, Theodore Roosevelt – mwanachama wa Freemason aliyekuwa amemaliza kwa mafanikio katika muda wake wa mihula miwili kama Rais ndani ya Ikulu ya Marekani.
Roosevelt alikuwa amekuja Afrika kwa mwaliko wa Taasisi ya Smithsonian ya Washington. Ziara yake ilisherehekewa zaidi kwa kumtunuku tuzo nyingi kuliko alivyotarajia kutoka kwenye taasisi ya kitaaluma.
Roosevelt aliteuliwa mwanachama wa heshima wa ofisi ya Freemason. Picha na sahihi yake bado vipo kwenye ofisi ya Nairobi.
Mfalme Arthur wa Connaught na Strathearn, alipoitembelea ofisi mwaka uliofuatia, alikuwa kiongozi mkuu wa ofisi ya Uingereza. Aliteuliwa Gavana mkuu wa ofisi ya Canada wakati alipopigiwa simu na ofisi ya Harmony.
Sarafu ya Rupia ya Waingereza wa Kihindi na fedha za noti zilianzishwa Zanzibar wakati huu. Gari la kwanza la Kijerumani la Daimler lilitumiwa na Sultani.
Magari aina ya Morris Cowley, Citreon na Fiat yaliingia Zanzibar na bara kipindi hicho. 
Mwaka 1911, mwaka ambao Sultani wa Zanzibar alihudhuria sherehe ya kumsimika Mfalme George V, ndiyo wakati ambapo ofisi ya Freemason tawi la Victoria Nyanza namba 3492 ilifunguliwa. Ilikuwa ya kwanza kufunguliwa Uganda.
Miaka miwili baadaye, ofisi ya Menengai namba 3559 na Mombasa namba 3645 zilifunguliwa. Mwanzoni mwa Vita ya Kwanza ya Dunia mwaka 1914, jumla ya ofisi saba zilikuwa zimeshafunguliwa chini ya Katiba ya Kiingereza huku idadi ya wanachama ikikaribia mamia.
Vita ya dunia ilikwamisha maendeleo ya Freemason baada ya vijana wadogo wa Kiingereza kuingizwa jeshini. Pingamizi liliwekwa na vijana huko Zanzibar mwaka 1918. Ofisi ya pili ya Freemason ilifunguliwa Novemba 15 mwaka ule. 
Matokeo ya vita hayakuruhusu ofisi ya Zanzibar namba 3897 kusimikwa rasmi hadi Machi 29, 1920.
Gari la kwanza la mizigo tani mbili lilinunuliwa wakati ule, ambalo lilikuwa chini ya Idara ya kazi ya jamii.
Idara ya Kimataifa ya masuala ya bahari ilifanya kazi kati ya mwaka 1892 hadi 1920. Kituo cha kwanza cha kizani kilizinduliwa mwaka 1923 huku Serikali na Bunge la kwanza likirasimishwa mwaka 1926.
Kuondoka kwa utawala wa Kijerumani bara, kulichochea uanzishwaji wa ofisi za Freemason. Ofisi ya kwanza ya Freemason ilianzishwa Tabora na baadaye kuhamishiwa Dar es Salaam kwa ajili ya kuwasaidia askari wa Kiingereza. 
Ofisi iliyojulikana kama mbingu ya amani namba 4835 ilianzishwa. Wanachama wake waliwakilisha jamii ya Watanganyika ambao walitarajiwa kuwa na tabia za Kiingereza.Itaendelea..........
MWANANCHI

TAPELI WA MAPENZI (STORI YA KWELI)



Peter ni kijana mwenye umri wa miaka 19,ambaye anaishi pamoja na wazazi wake wote wawili.Ni kijana anaependa sana mambo ya kileo na hasa kukaa kwenye vijiwe na marafiki ambao wapo sawa na ki umri, mara nyingi hapo kijiweni huwa mada yao kubwa sana ni kuzungumzia WASICHANA Na hata wakipita huwajadili.

Peter ni mtu anayependa masifa sana na kujigamba akiwapo na rafiki zake kijiweni.Mara nyingi hupenda kuwasimamisha wanawake kadhaa wapitapo karibu na kijiwe chao.

Siku moja Peter akiwa ame keti kijiwen akiwa na rafiki zake, alipita msichana moja aitwae HUSNA.Alimwita na kumwambia asimame,alipo simama Peter akamsogelea na kuanza kumuelezea shida yake ya kuwa anampenda na hatimaye akafanikiwa kupata namba za simu za husna.

Usiku wake Peter alimpigia Husna na kutaka kujua hatima ya jibu lake sababu aliambiwa asubiri ili afikiriwe jibu lake.

Kutokana na u Handsome alokuwa nao musa, husna hakuweza kuwa na hiyana tena juu ya kumkubali Peter kuwa wapenzi.

Peter akifurahi sana juu ya kujiba amekubaliwa na Husna kuwa wapenzi! 

Katika mapenzi yao walikaa kwa muda wa wiki moja, husna alipata alichokuwa anakihitaji kutoka kwa Peter! kiukweli alikuwa anajisikia vizuri sana kuwa na peter! baada ya wiki ile kuisha peter alimpigia Simu husna na kumwambia wakutane kijiweni Anataka kumpa suprice nzuri sana Husna.
Kwa kuwa Husna alisha zoea kupewa anachotaka kutoka kwa peter alikubali wakutane,

Ilikuwa ni siku ya Jumaa mosi majira ya saa 12 jion kweli husna alikwenda hadi kijiweni! Kufika Alimkuta Peter akiwa anamsubiri.Walikaachini wakizungumza kwa muda wa dakika 5.Peter alimshika mikono Husna na kumnyajua juu. kisha akamwambia nifuate mimi ninapo elekea!

Peter alitangulia mbele husna akimfuta hadi kwenye chumba alichokuwa amekiandaa peter.
waliingia hadi ndani,Peter akafunga mlango kisha akaketi na Husna kitandani! Peter alianza kumwambia maneno mazito ya mahaba! husna huku akimpapasa husna mwili wake....

Baada ya Peter kumpapasa Husna mwili wake,akawa anamwambia wafanye Malavidavi pale.. husna hakuweza kukubali haraka haraka na badala yake akawa anagoma huku akimwambia Peter kwanin hakumtaarifu mapema Juu ya swala lile,, Peter aliduwaa kimya huku akimtumbulia macho Husna.Husna alizidi kugoma na kumwambia labda wafanye kesho yake!

peter alimbembeleza sana husna wafanye lakini aligoma kabisa.

Peter alikuwa ni mjanja sana,,,,mfukoni alikuwa na shilingi Elfu 1,500 akaamua kumlaghai Husna kuwa amsamehe kwa kuto mtaarifu. peter alimwambia husna "basi me sababu nakupenda ntakukipa elfu 15,000 Kama pesa ya usumbufu, alitoa shilingi elfu Zile 1500 na kumshikisha husna mkononi, zilikuwa ni noti tupu na ndani palikuwa ni giza san kiasi husna hakuweza kugundua kama zilipesa zilikuwa ni 1500 na sio elfu 15000 husna alilainika kabisa baada ya kupewa zile pesa mkononi.. na hatimaye alijikuta wakifanya mambo yetu yaleeeh!

wakiwa katikat ya mechi Peter alipeleka mikono hadi kwenye viganja vya husna na kuzitoa zile pesa......

Baada ya kuzitoa zile pesa alizompa,waliendelea kula malavidavi yao tu! peter alimpagawisha saana Husna kwa michezo hatar aliyokuwa akimpa!

ghafla walisikia mlango ukigongwa kwa nje! peter alitoka kitandani na kuelekea hadi mlangoni kufungua mlango kujua ni nani aliyekuwa anagonga! alifungua mlango na kumkuta Rafiki yake nje aitwa Festo. peter akamuuliza Festo kulikoni? festo akamwambia kwamba afanye upesi ili na yeye waingie na msichana wake.Peter akamuelewa Festo akamwambia sawa subiri dakika 10.Peter alifunga tena mlango nakurudi hadi kitandani.akamkuta Husna amekaa.

peter akamwambia Husna nyanyuka na uvaenguo zako! kweli Husna alifanya kama peter alivyo mwambia,, kisha alifungua mlango na kumwambia Husna atoke na aende hadi kijiweni amsubiri pale, husna alifanya hvyo. baada ya kuondoka husna Peter nayeye alipita njia yake na kukimbia nyumbani kwao.Husna akiwa amekaa kwa muda mwingi kijiweni bila ya Peter kutokea akaamua na yeye arudi kwao...

peter akiwa nyumbani kwao....

Peter akiwanyumbani kwao, husna alimtumia ujumbe peter ulikuwa hv! "Ndo nini kuniweka pale?" Peter alijitetea kwa kumjibu "samahani mpenzi, nilikuja kuitwa na rafiki yangu kwamba baba alikuja kunifua kijiweni sasa,alivyo nikosa akawaachia maagizo rafik zangu kuwa niende nyumbani haraka san kunakitua nikachukue nipeleke kwa shangazi ndo maana sikutokea!" husna alikubali kutokana kumuamin sana Peter!

SIR CHANDE: NILIVYOPATA UONGOZI FREEMASON


Dar es Salaam. Wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong’ono. Tumeona matangazo yakialika watu kujiunga nao kama wanataka kupata utajiri na kuwa watu wenye nguvu. Lakini bado Freemason, imebaki kuwa kitendawili miongoni mwa Watanzania wengi.

Leo tunakuletea habari kuhusu Mtanzania maarufu aliyefungua kinywa na kueleza namna alivyojiunga na Freemasons, kundi lililo kongwe duniani.

Tayari watu mbalimbali watu wenye hamu ya kupata utajiri wamekuwa wakitoa ushuhuda kuhusu kundi hilo na kusikika kwenye vyombo vya habari, hasa baada ya kifo cha mwingizaji nyota, Stephen Kanumba, mwaka 2012.

Siyo hivyo tu, bali kumeibuka pia matangazo yenye namba za simu yanayoshuhudiwa kwenye nguzo za simu mitaani hadi vichochoroni yakiwataka watu wanaotaka kujiunga na Freemason kupiga simu ili wapewe utaratibu wa namna ya kujiunga kwenye ‘kisima hicho cha mafanikio’.

Baadhi ya watu tayari wameshanaswa na mtego huo, huku wengine wakiendelea kujaribu bahati yao kujipatia utajiri kwa njia ya ‘nguvu za giza’.

Hata hivyo Jayantilal Keshavji Chande, maarufu zaidi nchini kwa jina Sir Andy Chande, aliyejiunga na Freemason Oktoba 25, 1954 baada ya kupita kwenye usaili mzito, anaeleza namna alivyoibuka kutoka familia ya kawaida hadi kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.

Sir Andy Chande, ambaye amekuwa mwanachama wa kundi hili kwa karibu miongo sita sasa, anaeleza namna alivyosajiliwa na kufikia hatua ya juu ndani ya kundi hilo.

Chande alizaliwa Mombasa Kenya, Mei 7, 1928, ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene mjini, mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania.

Katika kufafanua utaratibu mzima wa Freemason, Chande ameandika kitabu alichokiita; ‘A night in Africa-a journey from Bukene’ (Usiku wa Afrika-Safari kutoka Bukene), pengine akitaka kuweka sawa dhana na kuondoa tofauti ili misingi inayoendesha Freemason ifahamike.

Imani ya kimaadili na thamani ya kundi hilo ilianza wakati wa mazungumzo yake na Messrs Campbell Ritchie na McLean mwanzoni mwa miaka ya 1950.

“Katika kipindi kile nilianza kutambua kuwa Freemason ipo katika msingi wake. Ni sayansi ya maisha ambayo malengo yake ni kumbadilisha mtu kiimani na kumfanya awe anavyopaswa kuwa. Ni mabadiliko ya mtu binafsi,” Sir Andy Chande ameandika katika kitabu chake chenye kurasa 207.


Anasema kuwa malengo ya Freemason yamefunikwa na mafumbo, ambayo pengine ndiyo yanayoeleza utamaduni uliojificha katika utendaji kazi wake.

Chande anabainisha kuwa kanuni kubwa tatu za Freemason ziliandikwa kwenye kitabu kimoja nchini Canada, kilichochapishwa na Kampuni ya Penumbra Press.

Anaandika: “Kwa hiyo, ukiwa kwenye ngazi ya kwanza (first degree), kanuni inayoongoza, inamtaka mtu awe mkweli na mwenye maadili ambayo hasa Freemason inalenga kuyaweka kwenye akili, ili mwanachama awe mzuri.
Ngazi ya pili ya utaratibu inatilia mkazo kwenye vipaji na akili kupitia sanaa na sayansi, ili kutoa mchango mzuri iwezekanavyo kwenye maisha.”

Anafafanua kuwa ngazi ya tatu inampa mtu nafasi ya kutafakari uwepo wake kwa kina na kwamba kanuni zote tatu zinafahamika kama upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli.

“Kwa njia hizi inamaanisha, unafundishwa namna ya kuyafurahia maisha kwa kiwango chake cha juu. Kwa kufuata hizo kanuni tatu za upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli, wakati huohuo ukijitambua na kuanza kujiandaa na kutokwepeka kwa kifo,” anaandika Chande.

Anaongeza kuwa, wakati kanuni hizo tatu zinapoondolewa kwenye alama ya sanaa inayofunika imani ya Freemason, ambazo zilimpa udadisi wa kupata taarifa kuhusu utaratibu huo wa kale.
Sir Andy Chande ni Kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.
Kanuni za Freemason zinafundisha nini?

Katika ratiba ya Freemason, anaandika Chande akieleza kuwa, kanuni ya upendo wa kindugu inawafundisha ndugu wote kuwachukulia wanadamu wote kama familia moja iliyoumbwa na nafsi moja kuu.

“Kujiweka huru, vilevile, inaleta ujumbe nilioupata kutoka kwa baba yangu, aliyesema ni kuwekwa huru kwa mtu mwenye msongo. Kama ni kuwekwa huru kutoka kwenye umaskini, matatizo au akili isiyo na furaha,” anaandika Chande katika kitabu hicho.

Anafafanua kuwa ngazi ya tatu ambayo ni ukweli na pengine ndiyo muhimu zaidi ni mchango wa kimungu kwa mwanachama wa Freemason.

Anabainisha kuwa kipindi hicho ndicho kinachoheshimika kama njia ya matazamio na marekebisho na kama inawezekana, kurudiwa kwa kanuni hizo kama msingi wa kuelekea kanuni kuu nne alizozitaja kuwa ni; udhibiti binafsi, nguvu, umakini na haki.

Chande anaeleza kuwa Freemason siyo kifaa cha dini, pia siyo mpinzani wa dini, lakini inakaribisha watu wote bila kujali dini zao na haijaribu kubadilisha imani zao au kushawishi kuabudu kwao.

“Inajaribu tu kuwafanya watu kuwa wema,” anaandika Sir Chande akifafanua:


“Hii ndiyo dunia niliyoingizwa mwaka 1954, imekuwa na mchango mkubwa katika maisha yangu tangu wakati huo…: Roho yangu, akili yangu na nafsi yangu, vimetajirishwa na kushiriki kwangu Freemason.

MWANANCHI